• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yauhimiza Umoja wa Ulaya kutekeleza makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2019-06-11 09:22:02

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif amezihimiza nchi za Ulaya zilizosaini makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 (JCPOA) zitekeleze wajibu wao katika kuunga mkono maslahi ya kiuchumi ya nchi hiyo.

    Akizungumza na wanahabari akiwa na mwenzake wa Ujerumani Bw. Heiko Maas ambaye yuko ziarani nchini Iran, Bw. Zarif ameeleza matumaini yake kuwa, juhudi zinazofanywa na Ujerumani na washirika wengine katika kulinda makubaliano hayo "zitazaa matunda".

    Awali, Bw Maas alisema Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinafanya juhudi kuisaidia Iran kunufaika kiuchumi kutokana na makubaliano hayo.

    Mwezi Januari mwaka huu, Umoja wa Ulaya ulitangaza kuanzisha utaratibu maalumu wa malipo wa INSTEX, unaolenga kuhakikisha biashara na Iran na kukabiliana na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano hayo mwezi Mei mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako