• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wazitaka nchi za Afrika Mashariki kuwa na vigezo vya pamoja vya utoaji wa hewa ya ukaa kwenya magari

    (GMT+08:00) 2019-06-11 09:22:39

    Umoja wa Mataifa umezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa na vigezo vya pamoja vya utoaji wa hewa ya ukaa kwenya magari.

    Akizungumza katika kongamano la kusawazisha vigezo vya udhibiti wa utoaji wa hewa chafu inayotokana na magari lililofanyika mjini Nairobi, Kenya, Mkuu wa kitengo cha ubora wa hewa na usafiri kilicho chini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Bw. Rob de Jong amezihimiza nchi za Afrika Mashariki kuondoa magari ya zamani yanayotoa moshi mchafu na badala yake kutumia zaidi magari yasiyokuwa na uchafuzi.

    Wakati huohuo, Umoja wa Mataifa umeahidi kuunga mkono nchi wanachama kukumbatia miradi ya magari ya umeme. Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kanda ya Afrika Bibi Juliette Biao Koudenoukpo amesema Shirika hilo litaunga mkono nchi wanachama katika kuendeleza sera na kubadilishana uzoefu. amesema Umoja wa Mataifa unachukua hatua hiyo kutokana na kuwa usafiri endelevu unatoa fursa za maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira, ikiwemo afya bora, ajira, uwekezaji, ushiriki wa jamii na maisha bora ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako