• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua awamu ya pili ya Wiki ya Biashara ya China

    (GMT+08:00) 2019-06-11 09:39:58

    Awamu ya pili ya Wiki ya Biashara ya China imefunguliwa jana huko Nairobi nchini Kenya, na kupongezwa na wateja wa huko wanaotaka kununua bidhaa zenye ubora wa juu.

    Mshauri wa masuala ya uchumi na biashara katika Ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce pamoja na maofisa watendaji wa sekta binafsi ya huko wameshiriki kwenye shughuli hiyo ya siku tatu iliyoanza jana.

    Inakadiriwa kuwa maelfu ya watu kutoka Kenya na nchi jirani watashiriki kwenye Wiki ya Biashara ya China, ambapo bidhaa mbalimbali zikiwemo bidhaa za matumizi ya majumbani, vipuri vya magari, na mashine ya kilimo zitaonyeshwa na kuuzwa.

    Ofisa mtendaji wa shirikisho la viwanda na biashara nchini Kenya Nemaisa Kiereini amesema awamu ya pili ya Wiki ya Biashara ya China itawanufaisha watumiaji wa huko na wajasiriamali wanaotafuta wenzi wa kibiashara watakaowasaidia kuagiza bidhaa kutoka China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako