• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bidhaa gushi zachomwa

    (GMT+08:00) 2019-06-11 19:29:46

    Mamlaka ya Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa Tiba (TFDA), Kanda ya Magharibi imeteketeza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya Sh20.4milioni.

    Bidhaa hizo zimeteketezwa katika sehemu ya kuchomea taka ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora, Kitete.

    Akizungumzia bidhaa hizo, mkaguzi wa dawa wa Kanda ya Magharibi, Frederick Luyangi amesema ni bidhaa za kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

    Amesema bidhaa hizo zilizoteketezwa ni zile ambazo hazifai na zilizoondolewa sokoni.

    Alipoulizwa kuhusu wafanyabiashara waliokamatwa katika ukaguzi uliofanyika maeneo ya biashara za chakula, dawa za binadamu na mifugo, vipodozi na vifaa tiba amesema maduka matatu yamefungiwa huku wahusika wakifikishwa kwenye mkono wa sheria.

    Luyangi ameomba ushirikiano wa wananchi katika kuwafichua wafanyabiashara wanaokwenda kinyume na sheria kwa kuuza bidhaa zisizofaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako