• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa makala kwenye vyombo vya habari vya Kyrgyzstan

    (GMT+08:00) 2019-06-11 19:41:57

    Rais Xi Jinping leo ametoa makala kwenye gazeti la Slovo la Kyrgyzstan na shirika la habari la Kyrgyzstan Kabar. Makala hiyo yenye kichwa cha "Kutumai urafiki kati ya China na Kyrgyzstan ukuzwe na kuendelea daima", inasisitiza kuwa, China na Kyrgyzstan ni nchi jirani, urafiki wao wa jadi ni wa enzi na dahari. Tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, zimejenga mfano wa kuigwa wa uhusiano mpya wa kuheshimiana, kushirikiana kwa usawa na kunufaishana.

    Kwenye makala hiyo, rais Xi pia amesema anatumai kupitia ziara hiyo kushirikiana na rais Jeenbekov wa Kyrgyzstan kupanga mustakabali wa maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili, na kuongoza uhusiano huo na ushirikiano katika sekta mbalimbali uendelezwe kwenye kiwango kipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako