• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe imesema haiko tayari kutekeleza kikamilifu eneo la biashara huria la Afrika

    (GMT+08:00) 2019-06-11 19:45:24

    Zimbabwe imesema haiko tayari kutekeleza kikamilifu eneo la biashara huria la Afrika hadi itakapokamilisha maendeleo ya viwanda. Waziri wa viwanda na biashara wa nchi hiyo amesema, Zimbabwe itaweza kufanya hivyo baada ya miaka 15, ili iwe na uwezo wa kunufaika na soko linalotolewa na eneo hilo.

    Utekelezaji wa eneo la biashara huria la Afrika ulianza Mei 30 baada ya kuidhinishwa na nchi 22 ikiwa ni pamoja na Zimbabwe yenyewe. Eneo hilo linatarajiwa kuimarisha biashara ya ndani ya Afrika, na kuunda soko lenye watu bilioni 1.2 na thamani ya dola Trilioni 2.5.

    Amesema serikali imefanya mazungumzo ya lazima na wanachama wengine, ili kufanya nchi hiyo isiwe ni sehemu ya kubwaga bidhaa. Amesema Zimbabwe inajipanga ili kufanya makampuni yake yaweze kuzalisha bidhaa zenye nguvu ya ushindani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako