• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wapitisha azimio kuhusu watu waliopotea katika mapambano ya kisilaha

    (GMT+08:00) 2019-06-12 08:46:15

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lake la kwanza kuhusu watu waliopotea kwenye mapambano ya kisilaha.

    Kwa mujibu wa Azimio hilo Namba 2474, Baraza hilo limezitaka pande hasimu kwenye mapambano ya kisilaha zichukue hatua mwafaka kuzuia kupotea kwa watu kutokana na mapambano hayo, na kuruhusu kubadilishana habari za kifamilia, kulingana na wajibu wao wa kimataifa.

    Mkurugenzi wa operesheni wa Shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Bibi Reena Ghalani amesema kama mtu aliyepotea ni mhimili wa uchumi katika familia yake, athari yake itakuwa mbaya, kwa kuwa jamaa zake watakabiliwa na changamoto za kisheria, kiutawala na kiutamaduni.

    Wakati huohuo, balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuondoa vyanzo vya mapambano ya kisilaha ili kutatua suala la kupotea kwa watu kwenye mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako