• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatakiwa kuimarisha ushirikiano na China

    (GMT+08:00) 2019-06-12 09:08:51

    Rais wa Baraza la viwanda na biashara la mji wa Chililabombwe nchini Zambia Bw. Nelson Musonda amezitaka nchi za Afrika zitume maofisa wataalamu wa kiufundi nchini China kujifunza uzoefu wa China kuhusu mpango wa kiuchumi wa muda mrefu.

    Bw. Musonda amesema hivi sasa Zambia na nchi nyingine za kusini mwa Afrika zinakabiliwa na changamoto ya umeme usio na uhakika, hivyo ni muhimu kwa China kuanzisha vituo vya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji.

    Baadhi ya wakazi wa Chililabombwe wamesema China inashirikiana na Afrika katika kuimarisha maendeleo ya biashara na uchumi.

    China imekuwa rafiki kubwa wa Zambia, na hii inaonekana katika reli ya TAZARA, ambayo ilijengwa kwa ajili ya kufungua biashara kati ya Zambia na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako