• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wawahimiza watendaji wa kisiasa nchini Malawi ziimarishe amani baada ya uchaguzi uliofanyika karibuni

    (GMT+08:00) 2019-06-12 09:09:26
    Umoja wa Afrika wawahimiza watendaji wa kisiasa nchini Malawi ziimarishe amani baada ya uchaguzi uliofanyika karibuni

    Umoja wa Afrika jana umewahimiza watendaji wote wa kisiasa nchini Malawii waimarishe amani iliyopatikana baada ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

    Kwenye taarifa iliyotolewa jana, mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amevitaka vyama vya siasa nchini Malawi vitatue migongano yoyote kwa njia ya amani chini ya mfumo wa katiba na sheria.

    Tume ya waangalizi wa uchaguzi ya Umoja wa Afrika nchini Malawi iliyoongozwa na rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama imesema, uchaguzi uliofanyika tarehe 21 mwezi Mei nchini Malawi ulifanyika katika mazingira ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako