• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yawekeza katika sayansi na uvumbuzi ili kutimiza mpango wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-06-12 09:28:09

    Kenya itawekeza katika utafiti wa sayansi, teknolojia na uvumbuzi ili kutimiza mpango wa maendeleo wa serikali unaozingatia usalama wa chakula, utengenezaji bidhaa, nyumba za bei nafuu na upatikanaji wa huduma za afya kwa wote.

    Katibu mkuu wa idara ya elimu ya vyuo vikuu na utafiti ya nchi hiyo Bibi Collette Suda amesema, serikali itatumia teknolojia ya juu na uvumbuzi kutimiza ukuaji wa pamoja na ustawi.

    Amesema hayo katika uzinduzi wa utafiti muhimu wa taifa kwa mwaka 2018 hadi 2022 unaoweka kipaumbele katika kutumia ujuzi wa kisayansi na uvumbuzi kuharakisha ukuaji wa kiuchumi, utoaji wa nafasi za ajira na kuhimiza uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

    Pia amesema, serikali hiyo imewekeza katika utafiti na mfumo wa kiikolojia wa uvumbuzi ili kutatua changamoto maalumu zinazokabili jamii ikiwemo njaa, umaskini, maradhi na mazingira yanayozidi kuwa mbaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako