• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KARATE: Timu 18 zapigania ubingwa mashindano ya karate

    (GMT+08:00) 2019-06-12 09:48:33

    Mashindano ya karate ya ubingwa wa Gorjuru yameendelea jijini Nairobi nchini Kenya, mashindano hayo yalijumuisha wanakarate wa umri wa chini hadi watu wazima.

    Katika fainali ya kiwango cha watu wazima kwa wanawake, Judith Mbula, aliibuka wa kwanza na kushinda dhahabu. Olivia Gatwiri alipata fedha katika nafasi ya pili, huku Carolyne Karanja akipata medali ya Shaba.

    Na kwa upande wa wanaume, Julius Muya alipokea dhahabu . huku Michael Ngaruiya aliridhika na fedha, nae Stephen Romario akipata medali ya Shaba.

    Mchezo wa watoto wa kike wa miaka 6-8, Angela Wambui alipata dhahabu, Aizelene Njambi aliridhika na medali ya fedha, naye Sarah Mbuli alijishindia Shaba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako