• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aondoka kwenda ziarani nchini Kyrgyzstan na Tajikistan

    (GMT+08:00) 2019-06-12 19:49:11
    Rais Xi Jinping wa China leo ameondoka Beijing kuelekea Kyrgyzstan ambako atafanya ziara ya kiserikali nchini humo kutokana na mwaliko wa mwenyeji wake Rais Sooronbay Jeenbekovna, na atahudhuria mkutano wa 19 wa baraza la wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO mjini Bishkek.
    Na kutokana na mwaliko wa Rais Emomali Rahmon wa Tajikistan, rais Xi atafanya ziara ya kiserikali nchini Tajikistan ambako pia atahudhuria mkutano wa ushirikiano na hatua za kujenga kuaminiana barani Asia (CICA) utakaofanyika mjini Dushanbe.
    Rais Xi ameambatana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, na ujumbe wa maofisa waandamizi wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako