• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya-Maseneta waikabili Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati kuhusiana na kupanda kwa Bei ya Mafuta

  (GMT+08:00) 2019-06-12 20:09:05

  Kamati ya Bunge la Seneti nchini Kenya jana iliilaumu serikali kwa kupanda kwa bei za mafuta nchini Kenya kutokana na kutoza bidhaa hizo kiwango cha juu cha ushuru.

  Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Nyeri Ephraim Maina ilimwita Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Udhibiti wa Nishati Pavel Oimeke aeleze sababu za kupanda kwa kwa bei ya mafuta nchini Kenya ambapo bei ya bidhaa hiyo katika soko la kimataifa huwa imeshuka.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Pavel Oimeke aliiambia Tume ya Bunge la Seneti la Kenya kuwa kuwa bei ya mafuta ghafi katika soko la kimataifa na gharama za usambazaji ndiyo inayochangia kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo nchini Kenya.

  Aidha Oimeke aliwahakikishia maseneta kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati itahakikisha kuwa inashusha bei ya mafuta sambamba na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako