• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yavitaka vyombo vya habari kunukuu vizuri kauli za rais Putin juu ya mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-06-13 08:47:34

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema vyombo vya habari vinapaswa kunukuu vizuri kauli za rais Vladimir Putin wa Russia juu ya mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, na kwamba majaribio yoyote ya kuharibu uhusiano kati ya China na Russia hayatafanikiwa.

  Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, rais Putin alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani kwenye mkutano wa Baraza la uchumi la kimataifa uliofanyika wiki iliyopita mjini St. Petersburg, alijibu kwa kunukuu methali ya kichina inayosema "Wakati chui wakipigana, kima mjanja hukaa kando na kusubiri nani atashinda."

  Msemaji huyo amesisitiza kuwa China na Russia zote zinapinga kithabiti hatua za upande mmoja, sera za kujilinda kibiashara na vitendo vya ukandamizaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako