• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KIKAPU: Timu za Uganda, Tanzania zatua Rwanda

  (GMT+08:00) 2019-06-13 08:56:43

  Timu za taifa za mchezo wa kikapu za Tanzania na Uganda za wanaume na wanawake zimetua jijini Kigali Rwanda tayari kwa mashindano ya kanda ya tano ya Afrika kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 16.

  Mashindano hayo yanatambuliwa na shirikisho la kimataifa la mpira wa kikapu (FIBA) yatafanyika wiki nzima yatatumika kwa ajili ya kufuzu kwa mashindano ya Afrika kwa umri huo,.

  Rais wa shirikisho la mpira wa kikapu Rwanda (FERWABA) Desire Mugwiza amesema, timu ya wanaume ya Rwanda itapambana kusaka tiketi ya kushiriki mashindano ya U-16 ya Afrika kwa wanaume, wasichana wao tayari wamejihakikishia nafasi hiyo baada ya Rwanda kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Afrika yatakayofanyika mwezi Agosti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako