• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Fainali za kombe la dunia kwa wanawake- Marekani yatoa kipigo cha mbwa koko, yaitandika Thailand 13-0

  (GMT+08:00) 2019-06-13 09:15:10

  Mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake yanaendelea nchini Ufaransa, kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo uwanja wa Auguste-Delaune II jijini Paris, Timu ya taifa ya wanawake ya Marekani iliipiga kipigo cha mbwa koko timu ya taifa ya Thailand kwa jumla ya magoli 13-0 katika kundi F Unaweza ukasema ni kama mchezo wa netball lakini ndio soka.

  Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa jana, Sweden imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chile, Nigeria nao wamewaonyesha soka linavyochezwa Korea Kusini kwa kuwabandika goli 2-0, huku wenyeji Ufaransa ikiibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Norway, na Ujerumani ikiipiga Uhispania goli 1-0. Leo Australia itavaana na Brazil.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako