• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia yasema pande mbili za Sudan zimekubali kushikilia makubaliano ya awali

  (GMT+08:00) 2019-06-13 09:30:20

  Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia jana imesema, pande mbili za nchini Sudan zimekubali kushikilia makubaliano ya awali kuhusu miundo, mamlaka na majukumu ya serikali ya mpito.

  Wizara hiyo imetoa taarifa ikisema, maafikiano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo kati ya mwakilishi maalum wa Ethiopia kwenye suala la Sudan Mohamoud Dirir na pande mbalimbali za Sudan, kwa lengo la kutafuta utatuzi wa hali ya kisiasa nchini humo kwa njia ya amani.

  Wizara hiyo pia imesema, ikiwa ni sehemu ya maafikiano hayo, mazungumzo yataanza upya hivi karibuni ili kutatua migongano inayobaki, ikiwemo baraza la kiraia na masuala mengine husika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako