• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa korosho kukutana Mtwara Julai

    (GMT+08:00) 2019-06-13 19:39:18

    Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimeandaa Kongamano la wadau wa korosho litakalofanyika mkoani Mtwara Julai 12 na 13, 2019.

    Lengo la kongamano hilo ni kuongeza ushindani katika soko, ushawishi wa kuwekeza katika mnyororo wa thamani wa zao hilo ili kuongeza ajira na mapato.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa kituo hicho, Godfrey Mwambe amesema hatua hiyo inatokana na kupoteza ajira na mapato mengi nchini kupitia usafirishaji wa korosho nje ya nchi.

    TIC imesema kuwa tangu mwaka 2018, imekuwa ikitafuta mipango ya kuzuia korosho kwenda nje, ili kulinda ajira.

    Amebbainisha kuwa changamoto ya masoko katika zao hilo inahitaji kuwa na mwendelezo katika ufumbuzi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako