• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Norrsken yafungua kituo chake cha kwanza barani Afrika nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-06-13 19:41:37

    Kampuni ya Norrsken kutoka Sweden ambayo huendesha vituo vya biashara imefungua kituo chake cha kwanza barani Afrika nchini Rwanda.

    Kampuni hiyo inahudumia wajasiriamali 340 na kampuni 120 mjini Stockholm.

    Kituo cha Kigali ambacho ni cha pili cha kimataifa duniani kinatarajiwa kuisaidia Rwanda kupiga hatua muhimu kibiashara na ubunifu.

    Biashara zinazoendesha ndani ya Norrsken ni pamoja na za sekta ya kilimo, afya, fedha na chakula.

    Mkuu wa oparesheni wa Norrsken bwana Funda Sezgi, amesema uwekezaji wa Rwanda ni sehemu ya mpango wa miaka 10 wa kuwa na vituo katika maeneo 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako