• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asema China na India zinapaswa kuhimiza uhusiano ulio karibu zaidi wa wenzi wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-06-14 09:02:28

    Rais Xi Jinping wa China jana huko Bishkek alikutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi.

    Katika mkutano wao rais Xi alisema, China na India ni nchi mbili pekee za soko jipya zenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1, na ziko katika kipindi muhimu cha maendeleo ya kasi. Hivyo pande mbili zinapaswa kushikilia msingi wa kuwa fursa wala sio tishio kwa upande mwingine, kupanua njia za ushirikiano, kuimarisha ujenzi wa hali ya kuaminiana, kulinda kwa pamoja biashara huria na utaratibu wa pande nyingi, na kulinda haki halali ya maendeleo ya nchi zinazoendelea.

    Kwa upande wake Bw. Modi amesema, India inapenda kukaribisha mawasiliano ya ngazi ya juu na China, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kutatua migongano kati ya nchi hizo mbili kwa hatua mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako