• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kuongeza nguvu kwa urafiki wa watu na maendeleo ya pamoja ya SCO

    (GMT+08:00) 2019-06-14 19:45:29

    Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) unaofanyika katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek.

    Katika hotuba yake, rais Xi amesema, inapaswa kuheshimu tamaduni tofauti za nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, kuongeza nguvu za kudumu kwa urafiki wa watu wa nchi hizo na maendeleo ya pamoja. Pia inapaswa kuimarisha ushirikiano katika sekta za utamaduni, elimu, utalii, michezo na vyombo vya habari, na kuongeza mawasiliano kati ya wanawake na vijana, kuongeza kujiunga kwa raia na kuwanufaisha. Amesema China inaunga mkono kujenga eneo la kimataifa la majaribio ya matibabu huko Fangchenggang, mkoani Guangxi nchini China, na kuendelea kuhimiza ushirikiano wa uvumbuzi wa matibabu wa SCO.

    Rais Xi ameongeza kuwa, pande zote zinapaswa kutekeleza makubaliano ya ushirikiano yaliyoidhinishwa kwenye mkutano huo, na kutumia vizuri nguvu za jamii na kufanya ushirikiano wa mitaa uwe nuru mpya ya ushirikiano wa utamaduni na watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako