• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bima ya bodaboda kuwakinga abiria itaumiza wahudumu – wabunge

    (GMT+08:00) 2019-06-14 20:03:11

    Wabunge wa Kenya wamepinga pendekezo la serikali kwamba waendeshaji pikipiki za uchukuzi – bodaboda – watahitaji kuchukua bima ya kuwakinga abiria wao dhidi ya madhara kama vile ajali za kila mara.

    Walisema hatua hiyo itaua sekta hiyo ambayo imekuwa tegemeo kuu kwa Wakenya wasio na ajira zinginezo za kuwafaa, hususan, vijana.

    Kulingana na viongozi hao, wazo hilo lililotangazwa na Waziri wa Fedha Henry Rotich alipowasilisha taarifa ya bajeti bungeni Alhamisi, huenda likachangia kuzorota kwa usalama nchini.

    Hii ni kwa sababu wale ambao watalazimika kuacha biashara ya bodaboda kwa kushindwa kugharimia bima hiyo huenda wakaamua kujiingiza kwenye uhalifu "kujitafutia riziki." Bw Rotich alieleza kuwa ingawa sekta hiyo imeajiri vijana wengi kwa sababu hutumiwa na watu wengi, pikipiki hizo husababisha ajali nyingi ambazo zimeacha watu wengi na majeraha ya kudumu na hata ulemavu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako