• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mali za uhalifu za bil. 90/- zataifishwa

    (GMT+08:00) 2019-06-14 20:03:32
    Makamu wa rais wa Tanzania Bi Samia Hassan, amesema Serikali imetaifisha mali mbalimbali zilizotokana na uhalifu wa kupangwa wa kuvuka mipaka zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 90 katika sekta mbalimbali.

    Sekta hizo ni madini, maliasili, fedha hususani katika maeneo ya upatu (DECI) na maeneo mengine.

    Bi Samia amesema mafanikio hayo yametokana na Tanzania kufanya marekebisho makubwa katika sheria ya utaifishaji wa mali zitokanazo na uhalifu pamoja na sheria ya kuzuia utakatishaji wa fedha haramu.

    Alisema lengo la kufanya maboresho hayo ni kuhakikisha zinakuwa na ufanisi unaotakiwa katika kupambana na mbinu mpya za kihalifu, hasa katika makosa ya uhalifu wa kupangwa na mengine yanayovuka mipaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako