• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgao kwa sekta ya kilimo wadidimia

    (GMT+08:00) 2019-06-14 20:03:48
    Serikali ya Kenya imeamua kuitengea sekta ya kilimo Sh52 bilioni pekee kwenye bajeti.

    Hilo lilikuwa ni ongezeko la asilimia 0.3 pekee kutoka Sh45 bilioni mwaka wa kifedha wa 2018/2019.

    Kulingana na ripoti ya serikali, kilimo huchangia asilimia 34 ya mapato yote nchini Kenya, huajiri asilimia 70 ya wananchi na huchangia asilimia 80 ya bidhaa zote zinazouzwa nje kutoka nchini Kenya.

    Mgao huo ni kinyume cha mkakati wa kufufua na kukuza sekta ya kilimo 2019-2029, ambao kulingana na serikali, ni njia wazi ya kukabiliana na baa la njaa ya mara kwa mara nchini.

    Mojawapo ya mapendekezo katika mkakati huo ni kuanzishwa kwa mashamba 50 ya ekari 2,500 kila moja au zaidi katika mpango wa kutumia ekari 500,000 kwa kilimo nchini. Kwa miaka mingi, kilimo kiliaminika kuwa uti wa mgongo wa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako