• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nguvu kuongezwa utalii wa fukwe

    (GMT+08:00) 2019-06-14 20:04:04
    Tanzania inatarajia kuongeza nguvu katika utalii wa fukwe kwa kuanzisha safari za meli za kisasa katika bahari pamoja na kuanzisha utalii wa mikutano.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda amesema hali halisi inaonyesha kwamba utalii wa fukwe una nafasi kubwa ya kuinua uchumi kwa kuwa mara nyingi wageni wanaotembelea huwa na mazoea ya kurudi mara kwa mara tofauti na utalii mwingine wa kutembelea mbuga za wanyamapori.

    Alisema baadhi ya nchi zimeanza kutumia utalii wa meli kwa ajili ya vivutio ambavyo vipo katika fukwe, hivyo kuongeza idadi ya watalii na pia kukuza mapato.

    Alisema licha ya kuongeza nguvu katika utalii wa fukwe, pia serikali itaongeza aina nyingine ya utalii wa mikutano ya kimataifa.

    Prof. Mkenda alisema maonyesha ya kimataifa ya utalii ya Karibu-Kili Fair ni moja ya mkakati na ubunifu wa kusaidia kuchochea na kutangaza vivutio vilivyoko Tanzania.

    Alisema lengo la serikali ni kuongeza idadi ya watalii watakaokuja Tanzania kutoka milioni 1.3 hadi milioni 1.5

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako