• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na mwenzake wa Tajikistan Rakhmonov

    (GMT+08:00) 2019-06-16 19:02:05

    Rais Xi Jinping wa China jana mjini Dushanbe alifanya mazungumzo na mwenzake wa Tajikistan Emomali Rakhmonov.

    Rais Xi ameipongeza Tajikistan kwa kuandaa kwa mafanikio mkutano wa kilele wa tano kuhusu hatua za kuimarisha ushirikiano na kujenga uaminifu barani Asia CICA. Amesema uhusiano kati ya China na Tajikistan unaendelea kwa kasi tangu nchi mbili zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi miaka 27 iliyopita, China inapenda kuimarisha mpango wa jumla kuhusu uhusiano kati ya nchi mbili, kuinua kiwango cha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali, na kujenga kwa pamoja jumuiya ya maendeleo na usalama kati ya China na Tajikistan.

    Rais Xi amesisitiza kuwa nchi hizo zinapaswa kuhimiza kuunganisha ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mkakati wa maendeleo wa Tajikistan, kuimarisha ushirikiano kwenye sekta za mawasiliano ya miundombinu, nishati, kilimo, viwanda na nyinginezo. Pia amesema China inapenda kuimarisha mawasiliano na Tajikistan kwenye sekta za utamaduni, elimu na utalii.

    Rais Emomali Rakhmonov amesema nchi yake inapenda kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta za nishati, viwanda vya mafuta na kemikali, umeme wa nishati ya maji na ujenzi wa miundombinu, na kudumisha mawasiliano ya kijamii.

    Wakati huo huo, rais Xi jana alihudhuria hafla ya kutunukiwa nishani ya kifalme na mwenyeji wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako