• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jukwaa la kimataifa la Ukanda Mmoja na Njia Moja na Ushirikiano Mpya wa China na Afrika lafanyika nchini Misri

    (GMT+08:00) 2019-06-17 08:58:37

    Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Ukanda Mmoja na Njia Moja na Hatua za Ushirikiano Mpya kati ya China na Afrika umeanza jana mjini Cairo, Misri. Mkutano huo wa siku mbili umekutanisha watu 80 wakiwemo maofisa wa serikali, wajasiriamali, wataalama, wasomi na watafiti kutoka Nigeria, Kenya, China na Misri.

    Katika mkutano huo, wataalam na wasomi wamejadili kuinua viwanda vya China na Afrika kutokana na uhusiano kati ya uchumi wa Misri na ushirikiano wa China na Afrika na ushirikiano kati ya China na Misri chini ya mfumo wa Ukanda Mmoja na Njia Moja. Pia wamejadili mapinduzi ya kiviwanda, maendeleo ya elimu ya ufundi stadi katika nchi za Afrika na safari mpya ya ushirikiano katika ujenzi wa Ukanda mmoja na Njia Moja.

    Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, mshauri wa masuala ya kiuchumi katika ubalozi wa China nchini Misri Bw. Han Bing amesema, ufunguo wa mafanikio ya Ukanda Mmoja na Njia Moja ni kubadili mwelekeo wa amani na maendeleo, kushikilia kanuni ya kutimiza ukuaji wa pamoja kupitia majadiliano na uratibu. Amesema kutokana na mwelekeo wa sasa wa kupinga utandawazi na kuibuka kwa vitendo vya kujilinda, Ukanda Mmoja na Njia Moja umetoa sauti yenye nguvu dhidi ya vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara. Amesema katika miaka sita iliyopita, ushirikiano chini ya Ukanda Mmoja na Njia Moja umepata mafanikio makubwa. Thamani ya jumla ya biashara ya bidhaa kati ya China na nchi zilizoko kwenye Ukanda Mmoja na Njia Moja imezidi dola za kimarekani trilioni 5.

    Bw. Han amesema Misri ni mwenzi wa asili katika ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, akisema katika miaka ya karibuni, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Misri umeinuliwa katika ngazi mpya. Thamani ya biashara ya pande mbili na ubora wa biashara hiyo umeongezeka, na kwa mwaka jana, thamani ya jumla ilizidi dola za kimarekani bilioni 13.8, ikiwa ni rekodi ya juu zaidi. Amesema ushirikiano katika mambo ya fedha kati ya nchi hizo mbili umeendelea zaidi, akisema Wachina waliofanya utalii nchini Misri wamefikia laki nne mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 30.

    Ikiwa nchi mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa mwaka huu, Han amesema Misri imechukua nafasi muhimu katika kuinua ushirikiano wa China na Afrika ndani ya mfumo wa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja.

    Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja lilitolewa na China mwaka 2013, na linahusisha Njia ya Hariri ya Kiuchumi na Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21, ambalo inalenga kujenga mtandao wa biashara na miundombinu unaounganisha Asia na Ulaya, Afrika, na zaidi katika Njia ya Hariri ya biashara ya zama za kale.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako