• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa WHO aeleza matarajio mazuri kuhusu kupungua kwa ugonjwa wa Ebola, DRC

    (GMT+08:00) 2019-06-18 09:40:15

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza matarajio mazuri kuhusu mwelekeo wa kupungua kwa ugonjwa wa Ebola katika sehemu mbili zilizoathirika zaidi zilizoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Bw. Tedros ameyasema hayo mjini Uganda kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa na WHO pamoja na wizara ya afya ya Uganda. Amesema kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola inaonekana kupungua katika sehemu za Butembo na Katwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Wiki iliyopita Uganda ilitangaza mlipuko wa Ebola baada ya watu watatu kuthibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo.

    Nchini Kenya, serikali ya nchi hiyo imesema itaanza kuwafanyia uchunguzi abiria wote katika uwanja wa ndege wa kaunti ya Kisumu, ambao uko mpakani na Uganda, ili kugundua kama wana maambukizi ya Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako