• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wasomali wanaokabiliwa na njaa kuzidi milioni mbili

    (GMT+08:00) 2019-06-18 09:40:37

    Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa mambo ya kibinadamu OCHA imesema, idadi ya watu wanaokabiliwa na hatari ya njaa nchini Somalia itazidi milioni mbili hadi kufikia mwezi Julai, ikiwa imeongezeka kwa asilimia 29 ikilinganishwa na makadirio ya mwezi Februari.

    OCHA imesema kuchelewa kwa majira ya mvua na mafuriko vimeleta uharibifu kwa mazao ya chakula, miundombinu, nyumba na mifugo. Aidha imesema upungufu wa maji safi umeongeza hatari ya mlipuko wa magonjwa ya maji, huku mafuriko yakisababisha watu kupoteza makazi yao.

    Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa, mazao ya chakula nchini Somalia yatapungua kwa asilimia kati ya 40 na 50 haswa katika sehemu za kaskazini na kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako