• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Nyota ya Mbwana Samatta yazidi kungára awamia na vilabu kibao vya ulaya

    (GMT+08:00) 2019-06-18 09:42:25

    Klabu ya SS Lazio ya nchini Italia imeingia kwenye kipute cha kumnasa mshambuliaji kinara wa klabu ya Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta. Samatta ameng'ara sana msimu wa 2018/19 uliokwisha hivi karibuni akiiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya Ubelgiji baada ya miaka minane. Kwa upande wa timu ya Tanzania, Taifa Stars chini ya unahodha wa Samatta wamefuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kusubiri kwa miongo minne. Tayari Samatta amekwisha weka wazi kuwa hatarajii kurudi Genk msimu ujao, na ana ndoto za kuhamia katika ligi ya Primia ya England. Vilabu kadhaa vya England vikiwemo Brighton, Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley vimehusishwa kutaka kumsajili Samatta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako