• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UHAMISHO: Pogba atangaza kuondoka Man United

  (GMT+08:00) 2019-06-18 09:47:35

  Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amesema muda huu unaweza kuwa ni muafaka kwake kuhamia sehemu nyengine. Kiungo huyo kinara wa timu ya taifa ya Ufaransa, anahusishwa na kutaka kuhamia katika klabu kongwe na tajiri ya nchini Uhispania, Real Madrid. Pia klabu yake ya zamani, miamba ya Italia, Juventus, inahusishwa na mipango ya kutaka kumsajili. Kiungo huyo mwenye miaka 26, ambaye alikuwa pekee kutoka Man United kujumuishwa kwenye kikosi bora cha ligi kwa msimu ulioisha wa 2018/19, bado ana mkataba na United mpaka mwaka 2021. Japo kuna uwezekano wa kupata fedha nyingi, inaonekana kuwa uongozi wa Man United unaamini Pogba ataendelea kusalia katika uga wa Old Trafford msimu ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako