• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kupanua uwanja wa Ndege Songwe

    (GMT+08:00) 2019-06-20 18:36:44

    Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, amesema serikali inatarajia kupanua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (Sia), ili uhudumie ndege kubwa za mizigo na abiria wakati wote.

    Uwanja huo utapanuliwa kutoka kilomita mbili zinazotumika sasa hadi kufikia kilomita 3.3, hatua itakayofanikisha ndege kubwa kutua katika uwanja huo.

    Aliyasema hayo jijini Mbeya wakati wa kongamano la kuhamasisha uwekezaji katika kilimo cha mboga na matunda lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji (TIC), Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (Sagcot) na Shirikisho la Wakulima wa Mboga na Matunda (Taha).

    Alisema lengo la serikali ni kuwezesha ndege za mizigo kutua na kupaa kwa urahisi na kuwarahisishia wananchi kusafirisha bidhaa zao kwenda kwenye masoko yakiwamo ya matunda na mboga.

    Aidha, serikali inakusudia kuukarabati uwanja huo kwa kuweka taa ili kuwezesha ndege kutua na kupaa kwa wakati wote

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako