• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makumbusho Tanzania yatakiwa kukuza utalii kwa kujitangaza

    (GMT+08:00) 2019-06-20 18:37:05
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania , Prof. Adolf Mkenda, ameitaka Makumbusho ya Taifa kuanzisha kampeni ya kutangaza ndani na nje ya nchi vivutio mbalimbali ambavyo vinapatikana katika makumbusho zote yakiwamo masalia ya binadamu wa kale.

    Prof. Mkenda aliyasema hayo alipotembelea makumbusho hayo na kujionea urithi na hazina ya taifa ambao ni pamoja na mafuvu na masalia ya binadamu wa kale au zamadamu.

    Masalia hayo ni pamoja na Australopithecus, Afarensis, Zinjanthropus (paranthropus) boisei, Homo habilis, Homo erectus na Homo sapiens, yenye umri wa tangu miaka milioni 3.6 hadi miaka 200,000 iliyopita.

    Alisema matangazo kwenye runinga, redio na magazeti kuhusu vitu vinavyotunzwa Makumbusho ya Taifa, yatajenga uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa makumbusho na hivyo, kufanya watu wengi kuyatembelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako