• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya itafungua kituo cha kusambaza maua nchini China

    (GMT+08:00) 2019-06-20 18:38:24
    Kenya itafungua kituo cha kusambaza maua nchini China katika hatua mpya ya kuwezesha mauzo ya moja kwa moja kwenye soko la bara Asia.

    Waziri wa viwand Peter Munya amesema kituo hicho kitafunguliwa katia mji wa Changsha mkoa wa Hunan kusini mwa China kwa ushirikiano na kampuni ya Funfree International ya China

    Waziri munya anasema kufunguliwa kwa kituo hicho kutawezesha Kenya kuuza moja kwa moja maua yake kwenye soko la china na nchi jirani.

    Kiwango kikubwa cha maua ya Kenya hufika kwenye soko la China kwanza kupitia Uholanzi ambayo hununua bidhaa hiyo kwa bei nafuu na baadaye kuuuza kwenye masoko kote duniani kwa bei ya juu.

    Makubaliano ya kufunguliwa kwa kituo hicho yatatiwa saini wakati wa maonesho ya kwanza ya kiuchumi na biashara yatakayofanyika mjini Changsha kati ya 27 na 29 Juni.

    Waziri Munya ataongoza ujumbe wa serikali kwenda katika maonyesho hayo ambako poa Kenya itaonyesha bidhaa kama vile kahawa, chai na parachichi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako