Wazalishaji hao walisema bei ya sasa ni Sh. 3,000 ambayo ni ndogo ikilinganishwa na thamani ya kahawa duniani, na kwamba ongezeko la bei litawawezesha wakulima wa kahawa kuzalisha kwa wingi, kuzingatia ubora na kukuza pato lao na la taifa.
Aidha, wameomba kurudishiwa mfumo wa kuwakopesha pembejeo za kilimo ili waweze kuzalisha kahawa nyingi zaidi na yenye tija sokoni.
Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama vya Ushirika Uru Njari, Felix Masao , alitoa ombi hilo alipokuwa akizungumzia hali ya uzalishaji kahawa.
Alisema ikiwa wakuliwa watatazamwa kwa jicho la pekee wataleta mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuondoa umaskini kwa jamii.
Masao alisema licha ya kahawa kwa sasa kushuka bei, mwamko wa wakulima ni mkubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |