• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi Laikipia Kaskazini walia wawekezaji, wakulima wanabadili mikondo ya mito

    (GMT+08:00) 2019-06-21 17:21:06
    Wakazi wa Laikipia Kaskazini nchini Kenya wameiomba serikali kuweka sheria kali zitakazowazuia wawekezaji kuharibu mito iliyoko eneo hilo.

    Wanalalamika kwamba maji kwenye mito eneo hilo hutiririka msimu wa mvua pekee, kwa sababu ya kampuni na mashirika yanayofanya kilimo na ambayo hubadilisha mikondo yake wakati wa kiangazi.

    Wenyeji hao wanadai mkulima wa kiwango cha chini ndiye anaendelea kuumia na kusababisha Laikipia kuwa mojawapo ya kaunti zinazopokea chakula cha msaada kila mwaka.

    Chanzo cha maji ya mito hiyo ni Mlima Kenya, na wanaonya kwamba sheria maalum zisipowekwa kudhibiti ubadilishaji wa mikondo kiholela huenda wakakosa kufanya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako