• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazawa walalamikia kuumizwa na kodi

    (GMT+08:00) 2019-06-21 17:21:22
    Wawekezaji wazawa mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali ya Tanzania kuwaangalia na kuwapunguzia utitiri wa kodi unaowakwamisha.

    Wamesema lengo la kufanya hivyo ni kuimarisha uwekezaji pamoja na kutoa ajira kwa vijana ili kupunguza umaskini.

    Meneja Msaidizi wa Marenga Milis, Priva John, aliyejikita kwenye kuzalisha unga na vyakula vya nafaka, ameomba serikali iangalie namna ya kupunguza mrundikano wa kodi unaowakabili wawekezaji wa ndani.

    Mrundikano huo alisema unawakwamisha hasa wawekezaji wazawa wenye mitaji midogo.

    Alisema ikiwa serikali itapunguza kodi wazawa wataimarisha thamani za bidhaa wanazozalisha kwa kuwa na bei nafuu kwa wateja wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako