• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Taifa kukaza mkanda kwa sheria mpya ya kiwanda cha mafuta .

    (GMT+08:00) 2019-06-24 20:19:39

    Serikali inasema itaongeza uangalizi katika sekta ya mafuta na gesi ili kuhakikisha kuwa wakezaji wanatoa fursa zaidi kwa makampuni ya ndani ili kutekeleza Sheria mpya ya Petroli.

    Kenya inajitayarisha kuanza uzalishaji wa mafuta ambayo inatarajiwa kufanya Kenya nchi ya kuuza mafuta ifikapo mwaka 2022.

    Waziri wa Petroli na Madini Andrew Kamau amesema tayari wizara ilikuwa imeanza kutekeleza Sheria ya Petroli iliyotengenezwa hivi karibuni, ambayo inatarajiwa kuongeza fursa kwa makampuni ya Kenya.

    Hapo awali, sekta hiyo iliendeshwa chini ya sheria ya zamani ambayo haikuhitaji makampuni ya uzalishaji wa mafuta kuzingatia sana makampuni ya biashara ya Kenya.

    Sheria mpya, hata hivyo, ina sehemu nzima juu ya maudhui ya ndani na mafunzo, ambayo huweka majukumu fulani kwenye makampuni ya mafuta.

    Kamau amesema Sheria hiyo itaongeza kasi ya maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi ya ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako