• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wazalishaji wa Thai wanajaribu kuwekeza katika biashara ya kilimo Uganda

    (GMT+08:00) 2019-06-24 20:20:00

    Huduma za Taifa za Ushauri wa Kilimo (Naads) zitashirikiana na Thailand ili kukuza uchumi wa kilimo ili kuongeza uzalishaji wa kilimo.

    Dkt Samuel Mugasi, mkurugenzi mtendaji wa Naads, amesema kilimo kinaendelea kukabiliana na changamoto kadhaa kati yao, ukosefu wa mashine za kilimo za kisasa na za bei nafuu, ambazo huzuia uzalishaji.

    Thailand ina historia ndefu ya uzoefu katika kilimo cha mchele, miwa na mhogo, na ndiposa wanatafuta fursa Uganda.

    Shirikisho lina wazalishaji 157 hususan kushughulika na mashine za kilimo.

    Dkt. Mugasi amesema kuna soko kubwa la mashine za kilimo nchini Uganda, huku akifafanua kwamba Uganda ilikuwa na nia ya kuimarisha utafiti katika aina ya mchele na mafunzo ya wafanyakazi ili kuhakikisha kuongezeka kwa uzalishaji.

    Mfumo mpya wa kilimo ni juu ya ajenda katika serikali Uganda ili kuongeza uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako