• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Shirika la reli Kenya kuongeza mabehewa 40 ya kubeba abiria kwenye laini ya Ruiru

    (GMT+08:00) 2019-06-25 18:46:02

    Shirika la reli nchini Kenya limeongeza mabehewa 40 ya kubeba abiria kwenye laini ya kutoka Ruiru kwenda katikati mwa mji wa Nairobi.

    Shirika hilo limesema mabehewa hayo yataanza kufanya kazi mwezi ujao katika hatua ya kushughulikia idadi ya abiria inayoongezeka.

    Pia hatua hiyo inatarajiwa kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu ya Thika na kuokoa muda kwa wafanyakazi wa mjini.

    Aidha shirika hilo limesema limesema wasafiri wanaotumia treni hiyo wataongezeka kutoka 300,000 kwa mwezi hadi zaidi ya milioni 2 ndani ya miaka 2 ijayo.

    Mkurungezi wa shirika la reli Philip Mainga amesema sehemu ya kwanza ya mabehewa 20 yataanza kuhudumu Julai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako