• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda kulegeza masharti kwa wawekezaji wa China

    (GMT+08:00) 2019-06-25 18:46:23

    Serikali ya Uganda imesema itawapunguzia ushuru na kutoa ardhi bila malipo kwa baadhi ya wawekezaji wa China ili kusaidia kufungua nafasi zadi za ajira nchini humo.

    Waziri wa biashara Michael Werikhe Kafabusa wakati akihudhuria maonesho ya kimataifa ya kilimo mjini Beijing amesema upunguzaji wa ushuru na ulegezaji wa masharti utakuwa ni kwa sekta kama vile kilimo, madini utengenezaji bidhaa na utalii.

    Aidha waziri Werikhe amesema China na Uganda zinahitaji kupunguza mwanya wa bishara.

    Kwa sasa China inaagiza bidhaa za dola milioni 30 kutoka Uganda huku nayo Uganda ikiagiza kutoka China bidhaa za dola bilioni 1.7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako