• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wanaochakachua tumbaku Tanzania kuchukuliwa hatua

    (GMT+08:00) 2019-06-25 18:47:03

    Serikali ya Tanzania imesema kuwa, itawachukulia hatua za kisheria wakulima wa tumbaku ambao wamekuwa na tabia ya kuchanganya tumbakusafi na chafu kwa ajili ya kujipatia kipatao ambacho sio halali kwao.

    Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Anamringi Macha, wakati akizungumza na vyombo vya habari, na kusema kuwa hali hiyo imekuwa ikiharibu taswira ya Tanzania kuwa tumbaku chafu inayozalishwa inatoka katika mkoa wa kitumbaku Kahama.

    Aidha, Macha alizitaka mamlaka zinazosimamia zao hilo ikiwamo Bodi ya Tumbaku kuwachukulia hatua za kisheri wakulima ambao wamekuwa na tabia ya kufanya udanganyifu kwa kufunga tumbakusafi na chafu sehemu moja kwa lengo la kujinufaisha kwa maslahi yao binafsi.

    Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika KACU, Emmanuel Charahani, alikiri kuwapo kwa vitendo hivyo, ambavyo vimekuwa vikijitokeza kila msimu wa uuzaji wa tumbaku nakuongeza mwaka huu wamemkamata mkulima mmoja kutoka chama cha msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako