• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatangaza mpango wa kukarabati miundombinu ya barabara katika mji mkuu

    (GMT+08:00) 2019-06-26 09:27:00

    Tanzania imetangaza mpango wa kukarabati miundombinu ya barabara katika mji mkuu, kufuatia serikali ya nchi hiyo kuhamia katika mji wa kisiasa wa Dodoma.

    Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano nchini humo Bw. Elias Kwandikwa amesema, serikali imetenga dola milioni 16.5 za kimarekani kwa mradi huo.

    Amesema, umuhimu ni kuboresha miundombinu, sio tu katika mji huo bali katika kanda nzima, huku akiongeza kuwa watu wengi wametembelea mji huo tangu serikali ilipohamia mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako