• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Netanyahu afikiria kufuta uchaguzi mkuu wa Israel uliopangwa kufanyika Septemba

    (GMT+08:00) 2019-06-26 10:09:41

    Chama cha Likud kinachoongozwa na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kimesema waziri mkuu huyo anafikiria kufuta uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika Septemba, 17. Uchaguzi wa mapema wa Israel ulifanyika Aprili 9, lakini Netanyahu alishindwa kuunda muungano wenye wabunge wasiopungua 61 kati ya 120. Vyama vya mrengo wa kulia vilipata jumla ya viti 65 katika uchaguzi huu, lakini waziri wa ulinzi wa zamani Avigdor Lieberman, kiongozi wa chama cha Yisrael Beiteinu alikataa kujiunga na muungano huo, hivyo kusababisha bunge kuvunjwa na kufanyika uchaguzi mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako