• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China wakutana na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2019-06-26 10:33:06

    Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Yang Jiechi hapa Beijing amekutana na mawaziri wa mambo ya nje kutoka Sierra Leone, Equatorial Guinea, Afrika Kusini na Senegal.

    Wakati Bw. Yang alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Sierra Leone Bw. Nabeela Tunis alisema, mwaka jana rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Sierra Leone Julius Maada Bio walifikia makubaliano juu ya kuimarisha urafiki wa jadi na kupanua ushirikiano kwa pande zote. Amesema pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa na viongzi wa nchi hizo mbili na matokeo yaliyopatikana katika mkutano wa kilele wa FOCAC. Bw. Tunis ameishukuru China kwa kutoa msaada kwa shughuli za ujenzi wa miundombinu, matibabu na afya nchini Sierra Leone.

    Bw. Yang amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Guinea ya Ikweta Bw. Simeon Oyono Esono Angue akisema, pande mbili zitahimiza ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na utekelezaji wa makubaliano ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC nchini humo. Bw. Angue amesema, China siku zote inatoa msaada na uzoefu wa maendeleo kwa Guinea ya Ikweta, na bara la Afrika kwa ujumla.

    Bw. Yang pia amekutana na Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bi. Naledi Pandor akisema, chini ya ufuatiliaji na juhudi za marais wa nchi hizo mbili, uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika Kusini umeendelezwa kwa kina na kutoa mfano wa kuigwa kwa uhusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano kati ya Kusini na Kusini. Bi. Pandor amesema, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia moja" litaleta fursa kubwa kwa maendeleo ya Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla, na Afrika Kusini itaunga mkono na kushiriki kwenye pendekezo hilo.

    Wakati Bw. Yang alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Senegal Bw. Amadou Ba, alisema, pande mbili hizo zinatakiwa kuendelea kuungana mkono, kuhimiza ushirikiano wa uchumi na biashara kuendelezwa ufikie ngazi ya juu, kuzidisha mawasiliano ya kiutamaduni, huku zikifanya juhudi za pamoja kulinda mfumo wa pande nyingi, kutoa mchango katika kulinda maslahi ya pamoja ya China na Afrika pamoja na nchi zinazoendelea.

    Bw. Ba amesema, Senegal ikiwa nchi mwenyekiti wa upande wa Afrika wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, inapenda kuratibisha nchi wanachama wa Afrika kufanya juhudi pamoja na China katika kutekeleza "Hatua Nane" za FOCAC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako