• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na nchi za Afrika kunufaisha watu wao kupitia ushirikiano wa sifa bora zaidi

    (GMT+08:00) 2019-06-26 19:14:49

    Mkutano wa waratibu wa kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC ulifungwa jana hapa Beijing, ambapo wahusika wa pande mbili wameeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano huo. Wamesema pande mbili zitashirikiana kulinda hali yenye pande nyingi na biashara huria, kujenga uhusiano mpya wa kimataifa, na kunufaisha watu wa China na Afrika kwa kupitia ushirikiano wa sifa bora zaidi.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming amesema, pande mbili zimeamua kulinda kwa pamoja hali ya pande nyingi na biashara huria, kupinga hali ya kuwepo upande mmoja na kujilinda kibiashara, kulinda mfumo wa kimataifa ambao Umoja wa Mataifa ni kiini chake, kulinda maslahi ya jumla ya nchi zinazoendelea, kushirikiana kujenga uhusiano mpya wa kimataifa, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Mratibu wa nchi wanachama wa pamoja wa FOCAC ambaye pia ni mshauri wa mambo ya nje wa rais wa Senegal Bw. Oumar Demba Ba amesema, uhusiano na ushirikiano wa kiwenzi kati ya China na Afrika ni uhusiano wa uwajibikaji, hauhitaji pande nyingine kuutathmini, na pande mbili zinaweza kubeba wajibu kwa urafiki kati ya China na Afrika. Amesema inapaswa kuhimiza zaidi ushirikiano na hali ya kuamiana kati ya China na Afrika, kutimiza uwiano wa uhusiano wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako