• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi 35 kushiriki Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam,maarufu Sabasaba

    (GMT+08:00) 2019-06-26 19:19:44

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade),Edwin Rutareguka,amesema nchi 35 zimethibitisha kushiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,maarufu kama Sabasaba mwaka huu.

    Kaulimbiu ya Maonyesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam mwkaa huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda."

    Rutageruka amesema nchi zilizothibitisha kushiriki maonyesho ya mwaka huu ni pamoja na Botswana,Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo(DRC),Comoro,Italia,Indonesia,Ghana na India.

    Aidha alisema kampuni zimefikia asilimia 93.3 ,lengo likiwa ni kukamilisha asilimia 100 kwa sbabau ni fursa nzuri kwa watanzania kutangaza biashara zao katika kipindi hiki ambacho washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani watakuwapo.

    Wakati huohuo Rutageruka alisema Mamlaka yake inaendelea kuhamasisha na kuwasiliana na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali kwenda kuwekeza na kufanya biashara nchini Tanzania kwa kuwa mazingira ni mazuri.

    Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanatarajiwa kuanza tarehe 28 Juni hadi Julai 13,mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako