• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yatia saini mkataba wa ujenzi wa kituo kidogo cha kusindika mafuta ghafi

    (GMT+08:00) 2019-06-26 19:20:56

    Serikali ya Kenya imetia saini mkataba na kampuni tatu za uchimbaji mafuta kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kusindika mafuta ghafi.

    Wizara ya Petroli na Madini jana ilitangaza katika ukurasa wake wa Twitter kwamba imeshirikiana na kampuni ya Tullow Oil,Total na Africa Oil Corp kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kusindika mapipa 60,000 hadi 80,000 kwa siku.

    Wizara hiyo ilisema kuwa makubaliano ni utafutaji wa mafuta katika visima 10 BB na 13T katika bonde la Lokichar Kusini.

    Tangazo hilo limekuja mwezi mmoja baada ya Kampuni ya Uchimbaji mafuta ya Uingereza ya Tullow kupata vibali vya udhibiti kutoka Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira nchini Kenya kuanza uzalishaji mdogo wa mafuta ghafi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako