• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Chepkoech na Manangoi wathibitisha kushiriki mbio za Herculis

  (GMT+08:00) 2019-06-27 14:22:27

  Wakimbiaji nyota kutoka Kenya Beatrice Chepkoech na Elijah Manangoi wamethibitisha kushiriki mbio za mita 1,609 (maili moja) za Herculis mnamo Julai 11-12 mjini Monaco, michuano ambayo ni ya tisa ya Riadha za Diamond League. Waandaaji wamesema kwamba Chepkoech, ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji, atapata ushindani mkali. Atakabiliana na anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 1,500 Muethiopia Genzebe Dibaba pamoja na mzawa wa Ethiopia Sifan Hassan, ambaye ni mkimbiaji matata wa Uholanzi. Chepkoech alifuta rekodi ya dunia ya mbio za mita 3,000 kuruka maji na viunzi ya Mbahraini Ruth Jebet, ambaye alizaliwa Kenya, ya dakika 8:52.78 iliyokuwa imedumu tangu mwaka 2016 na kuweka 8:44.32 mwaka 2018. Na mfalme wa Riadha za Dunia za mita 1,500, Elijah Manangoi atashindania taji la Herculis la maili moja dhidi ya mshika rekodi ya dunia ya ukumbini Samuel Tefera na bingwa wa Olimpiki na Riadha za Ukumbini za mita 1,500, Matthew Centrowitz.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako