• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasambazaji vifaa vya ujenzi watakiwa kutuma maombi ya tenda kwa serikali

    (GMT+08:00) 2019-06-27 18:48:56

    Serikali ya Kenya imewataka wasambazaji vifaa vya ujenzi kutuma maombi ya tenda kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu unaotekelezwa na serikali.Serikali imewataka watu hao kutuma maombi hayo na kuweka bei ya vifaa wanavyotarajia kusambaza kwenye mradi huo ndani ya miaka miwili. Taarifa hiyo inakuja wiki moja tu baada ya waziri wa fedha Bw Henry Rotich kutenga bilioni 10.5 katika kufanikisha miradi ya serikali huku bilioni moja ikitengewa ujenzi wa nyumba za bei nafuu. Rotich amesema kati ya bilioni 10 bilioni 2.3 zitatumiwa kuwasaidia watumishi wa umma kununua nyumba kwa malipo ya pole pole. Katika mpango huo shilingi bilioni moja nyingine zimetengewa idara ya polisi na magereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako